Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud ametoa ombi la dharura la kutaka msaada wa kimataifa kwa wahanga waliojeruhiwa katika milipuko ya mabomu ya magari mwishoni mwa juma, ambayo yaligharimu maisha ya watu 100.

Maombi hayo ya Serikali, ni yale ya kuchangia damu huku makumi ya watu wakikusanyika nje ya hospitali katika mji mkuu wa Mogadishu, kutafuta habari za wanafamilia wao.

Jumamosi Oktoba 29, 2022 magari mawili yaliyokuwa yamejaza vilipuzi yalilipua dakika kadhaa karibu na makutano ya Zobe yenye shughuli nyingi, na kufuatiwa na milio ya risasi katika shambulio lililolenga Ofisi za Wizara ya Elimu ya Somalia.

Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, alipovitembelea vikosi vya nchi yake nchini Eritrea. Picha: Zakeriye Ahmed /Horn diplomat

Shambulio jingine kama hilo, lilitokea katika makutano yale yaliyokuwa na shughuli nyingi ambapo lori lililokuwa na vilipuzi lililipuliwa Oktoba 14, 2017 na kuua watu 512 na kujeruhi zaidi ya 290, tukio ambalo lilikuwa ni baya zaidi kuwahi kutokea katika nchi hiyo yenye machafuko.

Kundi la Al-Shabaab, lenye mafungamano na Al-Qaeda limedai kuhusika na mashambulizi hayo, likisema wapiganaji wake walikuwa wakilenga Ofisi za Wizara ya elimu pekee.

Kufuatia hatua hiyo, Ikulu ya White House ya jijini Newy York nchini Marekani, ililaani shambulio hilo baya la kigaidi huko Mogadishu na kusema wahusika wanapaswa kuchukuliwa hatua kali.

Nabi afunguka ubora wa Club Africain
Kenyatta ahofia usalama, Rais amuagiza Waziri