Jumla ya Wanajeshi 13 wa Burkina Faso wameuawa, baada ya kuvamiwa na watu wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wa jihadi katika Jimbo la Mashariki mwa nchi hiyo.

Wanajeshi wengine 4 wa vikosi vya ulinzi pia walijeruhiwa katika shambulio la hapo jana (Oktoba 30, 2022), kwenye barabara inayounganisha miji ya Fada N’Gourma na Natiaboani.

Wanajeshi wombolezaji, wakiwa na picha za baadhi ya wanajeshi 27 waliouawa walipokuwa wakisindikiza magari 207 kwenye msafara kwenye kambi ya kijeshi ya Jenerali Sangoule Lamizana huko Ouagadougou, Burkina Faso, Oktoba 8, 2022. Picha: AFP

Shambulio hilo, linatokea baada ya kundi lenye nguvu na linalojinadi kusaidia Uislamu na Waislamu (GSIM), lililo na mafungamano na Al-Qaeda, kudai kuwa lilifanya shambulio kwenye kambi ya kijeshi huko Djibo, na kuwaua wanajeshi 10 na kuwajeruhi wengine 50.

Burkina Faso, imeshuhudia mara mbili ndani ya muda wa mwaka mmoja mapinduzi ya kijeshi, na pia inakabiliwa na uasi uliodumu kwa karibu miaka saba, ambao umegharimu maisha ya maelfu ya watu na kuwalazimu wengine milioni mbili kuyakimbia makazi yao.

Kitenge: Ninajutia kosa langu, nimeigharimu timu
Wapinzani walitaka kunizika nikiwa hai: Rais asimulia