Umoja wa Afrika AU, umetoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano yanayoongezeka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huku Rais wa Angola Joao Lourenco akisema atamtuma Waziri wake wa Mambo ya Nje, Tete Antonio nchini DRC ili kupatanisha mzozo huo.

Rais mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta ambaye ni Mjumbe wa Umoja huo na Mpatanishi wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki kuhusu mzozo huo, amesema ana wasiwasi juu ya hali ya mashariki mwa Kongo, na kuzitaka pande zote kuheshimu sheria za kimataifa, usalama wa raia na utulivu katika mipaka ya nchi za ukanda huo.

Hata hivyo, hatua hiyo inajiri ikiwa siku chache baada ya DRC kumtimua Balozi wa Rwanda nchini humo, Vincent Karega kufuatia tuhuma za muda mrefu kuwa Kigali inawaunga mkono waasi wa M23.

Rwanda, ambayo inakanusha shutuma hizo imeelezea kusikitishwa kwake na uamuzi huo na kuongeza kuwa wanajeshi wake kwenye mpaka wa nchi hizo mbili wako kwenye tahadhari kubwa.

Sheikh aomba msaada wa dharula vifo vya watu 100
Young Africans yapewa mbinu mpya CAF