Shirika linalotetea haki za binadamu, Amnesty International limesema kuwa tangazo la mipango ya kuunda kikosi kazi ambacho kitaanza kuwasaka na kuwakamata watu ambao wanadhaniwa kuwa ni mashoga, au wenye mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja, kuanzia wiki ijayo, limezua taharuki katika jumuiya ya kimataifa.

Mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za binadamu, Amnesty International, katika Kanda ya Afrika Mashariki na nchi za Maziwa Makuu, Joan Nyanyuki amesema kuwa mkakati mzima wa kuwepo kikosi kazi ni lazima usitishwe mara moja kwani unachangia kuhamasisha chuki kati ya wananchi.

Amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa Tanzania imechagua kuchukua hatua hiyo hatari katika kukishughulikia kikundi ambacho tayari ni watu waliotengwa.

Aidha, amesema kuwa suala la kikosi kazi ni lazima lisitishwe mara moja kwani linachangia katika kuhamasisha chuki kati ya wanajamii. mashoga tayari wanakabiliwa na ubaguzi, vitisho na kushambuliwa bila ya kuwepo matamko ya chuki ya aina hii.

“Serikali ya Tanzania lazima ihakikishe kuwa hapana mtu yoyote, hasa wale walioko katika madaraka kama vile Paul Makonda, anatoa matamko au anachukua hatua kupandikiza chuki ambazo zinahatarisha maisha ya watu kwa sababu tu ya jinsia yao au maumbile yao,”amesema Nyanyuki

Majaliwa aridhishwa na ujenzi wa SGR
Peter Msigwa: Siuzi gari yangu, waliotangaza ni wahuni tu