Shirika la Haki za Binaadamu la Human Rights Watch limemlaumu Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sissi kwa kupitisha mpango wake wa mateso magerezani, kitu ambacho limepinga mpango huo.
Aidha, Shirika hilo limesema kuwa al-Sissi, anajaribu kutafuta utulivu kwa gharama yoyote na ameruhusu mateso kwa wafungwa na kuwawekea vizuizi mbalimbali ingawa katiba ya Misri inapiga marufuku vitendo vya mateso kwa wafungwa.
Rais huyo wa Misri ametoa idhini kwa polisi na maafisa wa usalama kutumia mateso wakati wowote wanapoona inafaa ili kuweza kupata ukweli kuhusu mashtaka yanayowakabili.
Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi wa masuala ya Mashariki ya Kati kwenye shirika hilo lenye makao yake Jijini New York, Joe Stork amesema kuwa kuruhusiwa kwa mfumo huo wa mateso kumewafanya raia kukosa haki yao ya msingi.
-
Korea Kaskazini kufanya majairibio zaidi ya makombora
-
Marekani yaishangaa Korea Kaskazini kutaka vita
-
Chebukati ateua tume mpya ya uchaguzi Kenya
Hata hivyo, Wafungwa wengi wanadaiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la Udugu wa Kiislamu, lililoibuka baada ya uasi wa mwaka 2011 uliomuondoa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Hosni Mubarak.