KATIKA kuongeza ubunifu wenye tija kwenye masuala ya uchumi na kuondokana na changamoto ya UVICO-19 unaoikabili Dunia,Shirika la Posta Tanzania (TPC) limewataka wafanyabiashara, wajasiriamali wa mtandao pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo kujisajili katika huduma ya duka mtandao.

Kaimu Posta Masta Mkuu wa TPC,  Macrice Mbodo amesema hayo Jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani

Amesema uzinduzi wa Duka mtandao utafanikisha mikakati ya shirika hilo kukuza uchumi na kujitegemea kwa kutumia lugha zaidi ya lugha 20 zinazotumiwa duniani bila kusahau lugha ya kiswahili.

Amesema kupitia uzinduzi rasmi wa duka hilo,wamekuja na huduma mpya tatu ambazo ni Posta Kiganjani, Vituo vya Huduma kwa wateja Pamoja na Duka Mtandao. 

Mbodo anasema huduma hiyo inategemea zaidi ushirikiano wa watanzania na kwamba  iwapo wizara na taasisi zote zitafungua vituo vya huduma pamoja posta ni wazi huduma nyingi wanazotoa zitapatikana kwa urahisi na kuongeza mapato yatayosaidia kukuza uchumi na kuondoa utegemezi.


“Kupitia huduma ya duka mtandao ambayo inasimamiwa na shirika la Posta Tanzania tumefanikiwa kupata zaidi ya Sh.milioni 300 huku Watanzania wengi wakiendelea kujisajili kutumia huduma hii, juhudi zetu ni kuhakikisha Watanzania wengi wanajiunga na duka mtandao ili kufanya biashara zao kwa gharama ndogo,”anaeleza.

Amesema, kupitia Shirika la Posta, mteja anaweza akanunua bidhaa tofauti kwa wakati mmoja na akalipia hapo hapo alipo na  atapelekewa hadi nyumbani.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Habari , Mawasiliano,Teknolojia na Habari Mhandisi Kundo Methew ambaye katika maadhimisho hayo amemwakilisha Waziri wa wizara hiyo, Dkt Ashatu Kijaji  ametumia nafasi hiyo kueleza Umma historia ya Shirika  la Posta Tanzania (TPC)na kueleza kuwa lilianzishwa mwaka 1994, ambapo hadi sasa linatoa huduma nchini kote na kujiunga na mashirika mengine zaidi ya 670  duniani.

Amesema, mafanikio ya biashara mtandaoni yapo mikononi mwa jamii  kwamba historia inaonesha kuwa shirika hilo katika miaka ya nyuma limeweza kufanya vizuri katika utoaji huduma jambo ambalo limechangia kufika kidigitali zaidi.

Twiga Stars kuivaa Malawi
Taifa Stars yatokota nyumbani