Timu ya Taifa ya Tanzania Wanawake ‘Twiga Stars’ itacheza dhidi ya Malawi katika mchezo wa Fainali wa Michuano ya Ukanda wa Kusini mwa Afrika ‘2021 COSAFA Women’s Championship’ dhidi ya Malawi.’

Malawi imetinga katika mchezo wa Fainali, kufuatia kuwafunga wenyeji wa michuano hiyo Afrika Kusini mabao 3-2, kwenye mchezo wa pili wa hatua ya Nusu Fainali uliochezwa leo Alkhamis (Oktoba 07) majira ya jioni, katika Uwanja wa Wolfson, mjini Port Elizabeth.

Mchezo wa Fainali umepangwa kuchezwa keshokuta Jumamosi (Oktoba 09) katika Uwanja Wolfson, mjini Port Elizabeth kuanzia saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Twiga Stars ilitangulia Fainali, kwa kuichapa Zambia katika mchezo wa Nusu Fainali ya kwanza uliopigwa leo Akhamis (Oktoba 07) majira ya mchana.

Hadi dakika 90 za mchezo huo zinakamilika, timu hizo zilikua zimefungana bao 1-1, na ndipo sheria ya mikwaju wa Penati ilipochukua mkondo wake.
Katika hatua hiyo Twiga Stars ilipata mikwaju mitatu huku wapinznai wao Zambia wakipata mikwaju miwili, na kuifanya Tanzania kusonga mbele.

Ali Kiba aweka rekodi ya kipekee Apple Music
Shirika la Posta lazindua duka la Mitandaoni