Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeshinda kuwika nyumbani, baada ya kukubali kupoteza mchezo wa mzunguuko wa tatu wa Kundi J, dhidi ya Benin.

Stars inayowania nafasi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2022, imepoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 1-0, na kuipa nafasi Benin kuongoza msimamo wa Kundi J, kwa kufikisha alama 7.

Stars inaendelea kuwa na alama 4, walizozivuna kwenye mchezo dhidi ya Madagascar waliokubali kichapo cha mabao 3-2, huku DR Congo wakilazmishwa sare ya 1-1 nyumbani kwao Lubumbashi, mwezi uliopita.

Bao la Bebin limepatikana katika dakika ya 76, kupitia kwa Steve Maunie, aliyetumia udhaifu wa upande wa kulia wa Stars uliokua unatumikiwa na Shomari Kibwana.

Stars watarejea tena dimbani mwishoni mwa juma hili kucheza mchezo wa mzunguuko wa nne wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022, kwa kuikabili Benin ugenini.

Shirika la Posta lazindua duka la Mitandaoni
Dira ya uchumi wa Buluu Zanzibar kuimarika