Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC leo Jumatano (Novemba 04), watashuka tena Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Namungo FC kwenye mchezo wa mzunguuko watano utakaopigwa majira ya saa 1:00 usiku.

Simba SC inakwenda kwenye mchezo huo, huku ikiwa na kumbukumbu ya kuambulia matokeo ya sare ya bila kufungana dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Kwa upande wa Namungo FC, mara ya mwisho kushuka dimbani ilikua dhidi ya Azam FC, ambapo walipoteza kwa kufungwa bao 1-0, Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Kufuatia hali hiyo, timu zote mbili zinahitaji ushindi katika mchezo wa leo, hali ambayo inadhihirisha mpambano utakua mkali na wa kuvutia.

Simba SC yenye alama 8 baada ya kushuka dimbani mara nne, inashika nafasi ya 4 kwenye msimamo wa Ligi Kuu, huku Namungo FC yenye alama 5 baada ya kushuka dimbani 4, ipo nafasi ya 11.

Khalid Aucho aikana Simba SC
Jay Z ajiunga tena na Instagram