Baada ya kusubiri kwa muda mrefu, hatimaye Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limepanga Makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu 2022/23.

Shughuli za upangaji Makundi ya Michuano hiyo zimefanyika mjini Cairo nchini Misri majira ya mchana kwa saa za Afrika Mashariki, huku Wawakilishi wa Tanzania Klabu ya Simba wakipangwa Kundi C.

Simba SC iliyokua Chungu cha Tatu, imepangwa na Klabu za Vipers SC (Uganda), AC Horoya (Guinea) na Raja Casablanca (Morocco).

Kundi A katika Michuano hiyo lina timu za Wydad Casablanca (Morocco), Petro Atletico (Angola) , AS Vita (DR Congo) na JS Kabylie (Algeria).

Kundi B: Al Ahly (Misri), Mamelodu Sundowns (Afrika Kusini), Al Hilal (Sudan) na Coton Sports (Cameroon).

Kundi D: Espérance de Tunis (Tunisia), Zamalek (Misri), CR Belouizdad (Algeria) na Al Merrikh (Sudan).

Young Africans yatupwa Tunisia, Mali, DR Congo Kombe la Shirikisho
Try Again: Simba SC ipo katika mikono salama