Uongozi wa Simba SC umesema hauna taarifa zozote kuhusu Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison kuwasilisha ombi la kutaka Barua ya Kumuachia (Release Letter), ili kumpa nafasi ya kuendelea na Maisha yake ya soka nje ya klabu hiyo ya Mismbazi.
Mwezi uliopita, Morrison alipewa ruhusa ya mapumziko na Uongozi wa Simba SC hadi mwishoni mwa msimu huu, kwa madai ya kwenda kumaliza matatizo yake ya kifamilia nchini kwao Ghana.
Mwenyekiti wa Simba SC Murtaza Magungu amesema, hawana taarifa za mchezaji huyo kuwasilisha ombi la kutaka Barua ya Kuachiwa, na wanashangazwa kuona taarifa hizo zikisambaa kwa kasi kubwa katika Mitandao ya Kijamii.
Mangungu amesema Simba SC inafahamu bado Morrison ni mchezaji wao halali, na hakuna mahala popote ambapo klabu hiyo iliwahi kuthibitisha imeachana naye.
“Morrison bado ni mchezaji wa Simba SC, tunashangazwa kuona taarifa za kutuomba Barua ya Kumuachia (Release Letter), tulimpa ruhusa ya kwenda kwao kwa ajili ya matatizo ya kifamilia,”
“Mkataba na Morrison na Simba SC bado haujakwisha, anaendelea kupata stahiki zake kama mtumishi mwingine wa klabu hii, hatujawahi kutoa taarifa popote kwamba hatutaendelea naye, na hatuna taarifa zozote za yeye kuwa kwenye mpango wa kusajiliwa na klabu nyingine.” Amesema Mwenyekiti wa Simba SC Murtaza Mangungu.
Mapema leo Jumanne (Juni 21) asubuhi, Mwandishi na Mchambuzi wa Michezo kupitia kituo cha Radio Clouds FM Shaffih Dauda alinukuliwa akisema: “Bernard Morrison anaomba release letter kwa Simba, lakini Simba hawana presha wanataka mpaka mkataba wake utamatike kisha wamkabidhi barua
Inasemekana kuna muda aliwaambia kuna klabu ya nje inamtaka, Simba wakamwambia watume offer yao watapokea ofa na watampa release letter
Taarifa za kuaminika ni kuwa anataka kujiunga na Yanga, Simba wanafahamu hilo kwahiyo hawana tatizo zaidi ya kusubiri mwisho wa mkataba”