Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema mchezo wa keshokutwa Alhamis (Juni 23) dhidi ya Mtibwa Sugar utatumika kama sehemu ya kumuaga Beki wa kati kutoka Ivory Coast Pascal Serge Wawa.

Simba SC itakua mwenyeji wa Mtibwa Sugar katika mchezo huo wa mzunguuko wa 28 wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22, utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam,.

Mapema leo Jumanne (Juni 21), Simba SC imethibitisha taarifa za kuachana na Wawa, kupitia vyanzo vya habari vya klabu hiyo, huku sababu ikitajwa kumalizika kwa mkataba baina ya pande hizo mbili.

Ahmed Ally naye ametumia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii kuandika taarifa za kuutumia mchezo wa Mtibwa Sugar kama sehemu ya kumuaga mchezaji huyo, aliyedumu kwenye kikosi cha Simba SC kwa misimu minne ya mafanikio.

Ahmed Ameandika: Wawa atacheza mchezo wake wa mwisho Juni 23, dhidi ya Mtibwa Sugar utakaofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambao tutatumia kumuaga rasmi. Wanasimba tujitokeze Kama tulivyofanya kwa left footer Bwalya?

Kabla ya hapo Simba SC kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii iliandika: ?????? ?????? ????

Baada ya kutumikia timu yetu kwa misimu minne, Pascal Wawa hatakuwa sehemu ya kikosi chetu cha msimu ujao.

Mkataba wake utamalizika mwisho wa mwezi huu na mchezo wa Alhamisi dhidi ya Mtibwa Sugar utakuwa mchezo wake wa mwisho.

#NguvuMoja

Dar es Salaam na Hamburg kuadhimisha miaka 12 ya mahusiano
Polisi feki kortini kwa 'kumdunda' Polisi halisi