Bodi ya Wakurugenzi Simba SC chini ya Mwenyekiti wake Salim Abdallah ‘Try Again’ wapo kwenye mpango wa kushusha mashine tatu mpya na baada ya hapo watafunga zoezi la usajili wa Dirisha Dogo.

Ukiachana na kuboresha eneo la Kiungo Mshambuliaji kwa kumleta, Saido Ntibazonkiza aliyeonyesha makali yake mchezo wa kwanza, Simba SC ilikuwa inataka kuleta mastraika wenye uwezo wa kufunga ambapo wanataka wawili au mmoja.

Uongozi wa Simba SC kuhakikisha timu hiyo inapata mshambuliaji mzuri chaguo la kwanza alikuwa kwa Kwame Opuku anayecheza kwa mkopo klabu ya Najran ya Saudia Arabia akitokea USM Alger na Algeria.

Aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez aliwahi kufanya mazungumzo na Kwame na hata alipoondoka kwenye nafasi hiyo viongozi wengine waliongea naye ikiwemo kukubaliana masuala ya kimaslahi akihitaji mshahara wa Dola za Merakani 5000 ambazo ni zaidi ya Shilingi Milioni 10 kwa pesa ya Kitanzania.

Usiku wa Jumatatu (Januari 02) viongozi hao wa juu wa Simba SC wakiwa kwenye kikao cha kujadili masuala usajili ilibainika, Opuku ameumia mguu wake wa kulia na vipimo vya awali vinaonyesha anatakuwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kisichopungua mwezi mmoja.

Opoku baada ya kuumia aliwasiliana na viongozi wa Simba ikiwemo kuwatumia karatasi zake za hospitali pamoja na kuwaomba wasisitishe mpango wao.

Watatu akiwemo afisa wa Polisi kizimbani kwa uhaini
Afande Sele apinga ujio wa Kocha Robertinho