Afisa Mtendaji Mkuu wa Young Africans, Senzo Mazingiza Mbatha amethibitisha klabu hiyo itaingia kwenye windo la usajili wa Mshambuliaji wakati wa Dirisha Dogo.

Kiongozi huyo amethibitisha kuingia kwenye windo hilo, huku Dirisha Dogo likitarajiwa kufunguliwa rasmi kesho Jumatano (Desemba 15) na kufungwa Januari 15.

Senzo amesema dhumuni kubwa la kusaka saini ya Mshambuliaji wakati wa Dirisha Dogo limekuja, kufuatia kuumia kwa Mshambuliaji wao kutoka Burkina Fasso Yacouba Songne.

Songne alifanyiwa upasuaji wa goti mwezi Novemba, baada ya kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting Novemba 02, na tayari imefahamika hataweza kucheza sehemu ya msimu iliyosalia.

“Ikifika Dirisha Dongo nina amini kwamba tutafanya usajili lakini sio mkubwa sana, tuna mchezaji kama Yacouba (Songne) huyu aliumia, hivyo tutafanya utaratibu kumpata mchezaji mwingine ambaye atakuja kuziba nafasi yake.”

“Unajua kikosi imara kinahitaji wachezaji wazuri na kwa namna tulivyo kila mchezaji yupo bora jambo hilo linaonekana kwani hatuna hofu tunapoingia uwanjani kucheza na timu pinzani kwa namna yoyote ile kwa kuwa kila mchezaji ana uwezo mkubwa,” amesema Senzo.

Young Africans inaongoza Msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 20, ikifuatiwa na Simba SC yenye alama 18, huku kila mmoja akicheza michezo minane.

Koffi Olomide ahukumiwa miezi 18 jela
Chama, RS Berkane wakubaliana