Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa chama cha mapinduzi (CCM), Sophia Simba kwa mara ya kwanza amezungumza baada ya chama kumrudisha kundini ili aweze kuungana na wanachama wenzake.
Sophia Simba amesema kuwa ni mapema mno kwa yeye kuzungumza zaidi lakini kikubwa anashukuru kwa chama kumrudisha kundini mara baada ya kuomba radhi mara kwa mara ili aweze kusamehewa.
“Siwezi kuzungumza chochote kwani ni mapema mno kwangu, ila nashukuru Mungu kwa lililotokea, imekuwa ni muda mrefu sasa nilikuwa nje ya mfumo wa chama changu,” amesema Sophia Simba
Hata hivyo, Sophia Simba alivuliwa uanachama wa CCM kutokana na utovu wa nidhamu, lakini leo chama kimeamua kumsamehe na kumrudisha baada ya kuandika barua kadhaa za kuomba radhi, zilizosomwa hadharani na Rais Dkt. Magufuli