Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema, Patrick Ole- Sosopi amemtaka Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Utamaduni Juliana Shonza kutengua adhabu aliyompa Roma Mkatoliki kupitia wimbo wake wa Kibamia ya kumfungia miezi sita.

Sosopi amesema kuwa Sheria haimpi naibu waziri huyo mamlaka ya kufungia wasanii kujihusisha na muziki badala yake amesema wajibu huo upo chini ya Basata.

Ameongeza kuwa hakuna mtu anayependa kusikia au kuona nyimbo zenye maudhui mabaya lakini anashangaza na jinsi baraza hilo linavyofanya kazi kwa mashinikizo huku akiongeza kwamba adhabu zilizotolewa kwa wasanii hazistaili.

Hata hivyo ameendelea kwa kusema nyimbo hizo tayari zimeshasikilizwa kwa muda mrefu ni dhahili kuwa maadili na jamii zimeshapotoshwa kutokana na uzembe wa viongozi waliopaswa kuchukua hatua za haraka pindi nyimbo hizo zilipotoka.

Aidha, amesema Baraza la Sanaa la Taifa linapaswa kuchukuwa hatua kwa kushindwa kusimamia majukumu ya kazi zao ndiyo maana walishindwa kuzichukulia hatua nyimbo zinazodaiwa kutokuwa na maadili.

Amesema hayo jana pindi alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari.

 

Mwanajeshi wa JWTZ ahukumiwa kwenda jela
Tanzania yazijibu Marekani, Umoja wa Ulaya kuhusu hali ya usalama nchini.