Klabu ya Tottenham inatarajia kushuka dimbani kumenyana na Manchester United bila kuwa na mshambuliaji Harry Kane baada ya mchezaji huyo kupata jeraha la goti.

Kane mwenye umri wa miaka 24 ndio mfungaji wa mabao anayeongoza katika ligi ya Uingereza msimu huu akiwa na mabao 8 na alifunga mabao mawili wakati Spurs ilipoishinda Liverpool 4-1 siku ya Jumapili kabla ya kutolewa katika dakika ya 88.

Kutokuwepo kwa Harry Kane ni wazi kuwa litakuwa pigo kwa Spurs kwani mchezaji huyo yuko katika kiwango cha juu kwa sasa lakini ikumbukwe msimu uliopita Spurs walicheza mechi 8 za ligi bila Kane, wakishinda 5 na sare 3. wakifunga magoli 13 katika mechi hizo.

 

Kane amefunga mabao 13 katika mechi 12 za mashindano yote msimu huu huku Spurs ikiwa katika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Manchester United ni wa pili katika wakiwa sawa kwa alama na Spurs wakitofautiana magoli.

United wanaingia katika mchezo huu wakiwa wametoka kushinda mchezo wa raundi ya 6 ya Carabao Cup vs Swansea City baada ya kufungwa na Huddersfield wikiendi iliyopita.

Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 28, 2017
Video: JPM awataka wateule wake kufanyakazi kwa juhudi na weledi