Kamati ya Taifa Stars kupitia Mwenyekiti wake, Farouk Baghoza imeahidi kiasi cha shilingi milioni 500 endapo timu hiyo itaitoa Algeria usiku wa leona kufanikiwa kusonga mbele kuelekea katika hatua ya makundi ya kuwania nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2018.

Taarifa zinaeleza kwamba tayari kamati hiyo imetoa kitita cha shilingi milioni 25 kwa wachezaji wa Taifa Stars baada ya sare ya bao 2-2 dhidi ya Algeria.

Awali kamati hiyo iliahidi kitita cha Sh milioni 50 kama ingeishinda Algeria. Lakini ikaambulia sare ya bao 2-2.

Lakini sasa kuna ahadi ya Sh milioni 500 ambayo imetolewa kama Stars itashinda au kupata sare itakayoivusha hadi hatua ya makundi.

Stars inatakiwa kushinda au sare ya kuanzia bao 3-3 ili iweze kusonga mbele.

Tayari kikosi cha Stars iko mjini Bilda, Algeria kwa ajili ya mechi hiyo itakayopigwa usiku wa leo kuanzia saa 3:15 kwa saa za Afrika Mashariki ambapo kwa Algeria itakuwa ni saa 1:15 usiku.

Angela Merkel Kuwa Shuhuda Ujerumani Vs Uholanzi
Mkwasa: Tupo Tayari Kwa Mapambano Mjini Blida