Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager leo usiku saa 1:15 kwa saa za Algeria, (sawa na saa 3:15 kwa saa za Afrika Mashariki) itashuka dimbani kuwakabili wenyeji Algeria katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Stars inashuka dimbani kusaka ushindi katika mchezo wa leo, utakaoipelekea kuweza kusonga mbele kwa hatua ya makundi, kufuatia kutoka sare y amabao 2-2 katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.

Jana jioni Taifa Stars ilifanya mazoezi jioni katika uwanja wa Mustapher Tchaker uliopo mjini Bilda utakaotumika kwa mchezo wa leo, ambapo wachezaji wote wapo katika hali nzuri na morali ni ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo.

Akiongea kuelekea kwenye mchezo wa leo, kocha mkuu wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa amesema anashukru vijana wake wote wapo salama, hakuna majeruhi kikubwa anachosubiri ni jioni kushuka uwanjani kusaka ushindi katika mchezo huo.

Mapema leo asubuhi, benchi la ufundi la Taifa Stars pamoja na wachezaji wake, wamefanya matembezi ya miguu kwa dakika 30 katika viunga vya mji wa Bilda, kuweka miili tayari kwa mechi ya jioni dhdi ya Mbweha wa Jangwani.

 

Stars Kutajirishwa Kama Wataing'oa Algeria
TFF YATANGAZA TENDA YA MSHAURI WA ELEKTRONIKI