Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), kwa kushirikiana na mzabuni wa tenda ya elektroniki benki ya CRDB, leo limetangaza tenda ya kumsaka mshauri wa mfumo wa Elektroniki (Consultant) kwa ajili ya  kupitia mapungufu yaliyopo katika mfumo wa uuzaji tiketi wa elektroniki katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania.

TFF imetangaza tenda hiyo ili kumpata mshauri wa mfumo huo wa tiketi za elektroniki, ambao ulisamishwa na serikali mapema mwaka huu mwezi Aprili.

Maombi ya tenda yawasilishwe katika ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam, kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 10 jioni siku za kazi Jumatatu mpaka Ijumaa.

Gharama ya fomu ya kuombea tenda ni shilingi laki moja (100,000), na mwisho wa maombi ni Disemba 17, 2015.

Mkwasa: Tupo Tayari Kwa Mapambano Mjini Blida
Mama wa Gaidi aliyejitoa Mhanga Ufaransa Amzungumzia Mwanae