Kocha Mkuu wa Al-Ittifaq, Steven Gerrard amemjia juu mmoja wa mchezaji wake baada ya kuondoka bila ruhusa kabla ya mechi yao dhidi ya Al-Feiha.

Kocha huyo alimlenga nyota wa timu hiyo, Mohammed Al-Kuwaykibi baada ya suluhu kwenye mchezo wa Saudi Pro League huku akifoka kutokana na kitendo chake.

Kwa mujibu wa ripoti mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alishindwa kuripoti kwenye mechi kwa sababu alikuwa amechoka sana, jambo ambalo Gerrard amechukizwa.

Lakini Gerrard alikasirika zaidi baada ya timu ya madaktari wa Al Etti-faq kuthibitisha mchezaji huyo yupo fiti kucheza.

Akizungumza na waandishi wa habari alisema: Amepanda gari lake na kuondoka bila ya ruhusa, alipimwa na daktari, dokta akasema yupo vizuri kufanya mazoezi lakini akaondoka akidai amechoka sana. Natafuta sababu kwa nini hakuwepo kuisaidia timu.”

Wakati huo huo, AI-Ittihad imempa sapoti kocha baada ya kutoa tamko rasmi kufuatia kauli ya Gerrard kuhusu nídhamu.

Taarifa hiyo iliandikwa: “Sio mara ya kwanza Muhammad Al-Kuwaykibi kutenda kosa kama hilo, kwenye mechi dhidi va A-Nassr alikosa mazoezi ya timu sababu kama hiyo.”

Al-Kuwaykibi alicheza mechi 11 za ligi lakini alitoa asisti moja tu na hakucheka na nyavu msimu huu. Al Ettifaq kwa sasa ipo nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ikizidiwa pointi 13 na vinara Al-Hilal.

Kocha mpya Coastal Union aahidi yanayopendeza
Rais Samia amedhamiria kuwaletea maendeleo - Dkt. Biteko