Mwigizaji wa kike, Regina Simons amemtuhumu muigizaji mkongwe wa filamu za mapigano, Steven Seagal kuwa alimbaka siku chache kabla ya kukamilika kwa filamu ya ‘On Deadly Ground’ ya mwaka 1994.

Simons amekuwa mwanamke wa kwanza kujitokeza kueleza jinsi alivyobakwa na muigizaji huyo baada ya kujitokeza wanawake kadhaa ambao walidai kunyanyaswa kingono na Seagal.

Mwanamke huyo amedai kuwa alipokuwa na miaka 18 wakati ambapo Steven Seagal alimualika nyumbani kwake huko Beverly Hills akidai kuwa kulikuwa na hafla fupi, lakini alipofika alijikuta yuko peke yake.

Anasema alipomuuliza aliambiwa wengine wameshaondoka na kwamba amechelewa kufika, hivyo akamkaribisha ndani ya chumba chake kisha kumparamia kama mkewe.

“Tulipofika chumbani tu alifunga mlango na kuanza kunibusu. Kabla sijajielewa akanivua nguo na kuanza kunibaka, sikuweza kufurukuta kwani alikuwa na mwili mkubwa mara tatu yangu,” msichana huyo ameiambia The Wrap.

“Wakati huo nilikuwa sijaanza masuala ya mapenzi hivyo niliumia sana, machozi yalitiririka lakini nikama nilipigwa ganzi mwilini,” aliongeza.

Simons amekoleza moto wa tuhuma za unyanyasaji wa kingono baada ya kuwa wa kwanza kudai alibakwa na msanii huyo huku wengine wakisimulia jinsi alivyotumia kete ya kuwaweka kwenye filamu kuwanyanyasa kingono nyumbani kwake.

Seagal hajajibu tuhuma hizo ingawa zimekuwa mada kubwa kwenye ulimwengu wa filamu.

RC Mghwira akabidhi msaada wa vifaa vya mawasiliano kwa Polisi
Wanawake Saudi Arabia waandika historia kwenye uwanja wa mpira