Beki wa klabu ya Everton, John Stones amelazimika kuwasilisha barua kwa uongozi wa klabu hiyo ili afanikishe azma ya kuhama Goodson Park na kujiunga na klabu ya Chelsea iliyoonyesha nia tjhabita ya kutaka kumsajili katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Stones, amelazimika kufanya hivyo, baada ya uongozi wa klabu ya Evertyon kukataa ofa zilizotumwa klabuni hapo na klabu ya Chelsea zaidi ya mara moja na jibu lililokua likitolewa mchezaji huyo hauzwi.

Chelsea walifikia hatua ya kutuma ofa ya paund million 30, ili kufanikisha usajili wa beki huyo mwenye umri wa miaka 21, lakini mambo yaliendelea kuwa magumu kwao.

Hatua hiyo iliwafanya viongozi wa Chelsea kusitisha mpango wa kumsajili beki huyo, huku wakiwamini huenda kuna taratibu nyingine zitachukuliwa na Stones ikiwepo ya kulazimika kuondoka.

Stones, alijiunga na klabu ya Everton akitokea Barnsley mwezi januari mwaka 2013 kwa ada ya uhamisho wa paund million 3, na kwa kipindi chote alichokaa Goodson Park ametengeneza uhusiano mzuri na beki mzoefu Phil Jagielka.

Meneja wa Everton, Roberto Martinez amethibitisha hatua ya kupokelewa kwa ombi la Stones la kutaka kuondoka na amesisitiza jambo la subra, ili kufahamu nini kitakachotokea siku kadhaa zijazo kabla ya dirisha la usajili halijafungwa Septemba mosi.

Selena Gomez Achoshwa Na Maswali Ya Justin Bieber
Balotelli Atoa Ahadi Ya Kupiga Kazi