Selena Gomez amechoshwa na maswali anayoulizwa kuhusu mpenzi wake wa zamani, Justin Bieber.

Mwimbaji huyo wa ‘Come & Get’ ameonesha kukwazwa na kitendo cha media kutumia muda mwingi kumuuliza maswali ya Justin Bieber na kuweka kando mambo muhimu yanayohusu muziki wake hasa wakati huu anapopanga kuachia album yake mpya.

Uvumilivu ulimshinda Selena pale jarida la The Sunday lilipochapisha mahojiano yake huku likitoa kipaumbele kwa nukuu zinazohusu mapenzi yake na Justin Bieber na kuacha mambo mengine ya muziki.

“Nimevunjwa moyo kuona mahojiano niliyofanya hivi karibuni yanaonekana yanafanana kabisa na mahojiano niliyofanya nilipokuwa na umri wa mika 16,” Selena alitweet.

“Nataka kuachia album…niko tayari sasa watu kunifahamu mimi ni nani. Andika Mimi ni nani na acha kuogopa kuwa haitaongeza idadi ya watu wanaotembelea tovuti yako,” aliongeza.

Video: Kardashians waizimia ‘Ojuelegba’ ya Wizkid
Stones Awasilisha Ombi La Kuondoka Goodson Park