Serikali ya Sudan, imesema haitaki mjumbe maalum wa umoja wa mataifa nchini humo, ambaye ni mpatanishi mkuu katika mazungumzo ya kumaliza vita kati ya jeshi la Sudan na kundi la kijeshi la RSF, na tayari Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres amefamishwa kuhusu uamuzi huo.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan inakuja ikiwa ni wiki chache baada ya kiongozi wa jeshi la Sudan Generali Abdel Fattah Burhan, kutaka Volker Parthes kuondolewa majukumu yake ya kuwa mpatanishi katika mzozo huo.

Tangu pril 15, jeshi la Sudan, likiongozwa na Burhan limekuwa likipigana na kikosi maalum cha jeshi cha RSF kinachoongozwa na Generali Mohmmed Hamdaan Dagalo, kila upande ukilenga kupata nguvu za kuongoza serikali.

Zaidi ya watu 860 wamefariki kutokana na vita hivyo, na muungano wa madaktari nchini Sudan umesema kwamba huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

Trump ashitakiwa kwa matumizi mabaya nyaraka za siri
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 10, 2023