Polisi wa jiji la Lagos nchini Nigeria, wanamshikilia mtu mmoja aitwaye Ochukwu Akpannu (26), akituhumiwa kumkata kwa panga mchungaji ambaye alimfanyia unabii wa uongo.

Wakithibitisha kutokea kwa tukio hilo, wamesema mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Mei, 2023 kwa kumkata mapanga mchungaji huyo wa Kanisa moja la Kizazi Kipya, Nabii Anayochukeu.

Wamesema, tukio hilo liliripotiwa na waumini ambao walikuwa jirani na eneo la Makao Makuu ya kanisa liitwalo Ijesha jijini Lagos.

Hata hivyo, mshitakiwa alidai kuwa wakati wa maombi, Pasta alimueleza kuwa anakaribia kumpoteza dada yake isipokuwa hali hiyo itatoweka kwa kumfanyia maombi hali ambayo haikufanikiwa na anatarajia kufikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Aliyedaka penati ya Pele afunguka, aonesha mpira wa tukio
Vita Ukraine: Afrika yawakutanisha Putin, Zelesnky