Edson Arantes do Nascimento, anayejulikana zaidi kwa jina lake la utani la Pelé, alikuwa mchezaji wa soka wa Brazil ambaye alicheza kama fowadi.

Enzi zake kisoka alizingatiwa sana kama mmoja wa wachezaji hatari na mkubwa wa wakati wote, akiwa miongoni mwa watu waliofanikiwa zaidi na maarufu katika soka karne ya 20.

Edson Arantes do Nascimento, Pele.

Pele, alijulikana sana kwa mchango wake wa ndani na nje ya uwanja ambapo gwiji huyo wa Brazil alishinda tuzo nyingi wakati akitum,ikia kipaji chake na aliendelea kuhamasisha michezo hata baada ya kustaafu.

Anabaki kuwa ni mchezaji pekee aliyeshinda mataji matatu ya Kombe la Dunia na pia mwenye uwezo wa kufunga mipira ya adhabu pamoja na ujanja wake na mpira iliyokufa na hili halitasahaulika.

Picha: Kushoto Pele akiwa uwanjani na kulia akiwa amebea makombe matatu ya Ubingwa wa Dunia.

Lakini leo katika simulizi hii tunamleta mmoja wa watu ambao aliweka historia kwa kuzuia mpira wa Pele yeye anaitwa Sebastiao Luiz Lourenco.

Yeye ndiye kipa pekee aliye hai ambaye mpaka sasa ambaye aliokoa penalti ya Pele miaka 70, wakati Pele akiionekana kuwa mchezaji bora zaidi kuwahi kucheza mchezo wa soka kwa sababu ya umahiri wake.

Kipa aliyepangua penati ya Pele, Sebastiao Luiz Lourenco akiwa ameshika mpira aliodaka pindi Pele alipopiga penati.

Sebastiao Luiz Lourenco alipata bahati ya kuokoa penalti hiyo ya Pele katika mchezo wa ubingwa wa kitaifa wa Brazil kati ya timu ya Sao Bento waliopoteza mchezo dhidi ya Santos ya Pele, lakini Sebastiao Lourenco alifurahi kuokoa penalti ile ya Pele hadi leo.

Kwa upande mwingine, tambua kwamba Sebastiao Lourenco, ambaye sasa ana umri wa miaka 81, ameuhifadhi mpira wa mechi hiyo, iliyofanyika mwaka 1971 hadi sasa kama kumbukumbu na anasema ana furaha sana.

Picha: Kushoto ni Sebastiao Luiz Lourenco na kulia ni mpira wa kumbukumbu aliouhifadhi.

Siku ya tukio

Mei 12, 1971, Santos FC ya Pele na Sao Bento ya Sebastiao Luiz Lourenco walikabiliana katika Mashindano ya Paulista ya Brazil na licha ya timu ya Pele kushinda mechi hiyo, Sebastiao Luiz aliokoa mkwaju wa penalti kutoka kwa Pele.

Akiwa na shauku kubwa ya kuokoa mkwaju wa penalti kutoka kwa Pele, Sebastiao Luiz aliuchukua mpira huo mwisho wa mchezo na ameuhifadhi tangu wakati huo na Pele aliandika maandishi ya kukumbukwa kwenye mpira.

Lourenco ndiye kipa pekee aliye hai aliyepangua kiki kutoka kwa Pele na anasema yeye na Pele walianza kucheza kwa wakati mmoja, akiwa na umri wa miaka 15.

Lakini hata hivyo, Miaka 51 baadaye baada ya pambano lisilosahaulika kati ya wachezaji wote wawili, Pele aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 82 baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

Mbrazil Sebastiao Luiz Lourenco.

Ili kutoa heshima yake ya mwisho kwa mpinzani wake, Mbrazil Sebastiao Luiz Lourenco alipiga picha na mpira wa mechi yao ya mwaka 1971. kwasasa ana umri wa miaka 81 akiwa ni kati ya wanasoka wachache wa umri wa Pele ambao bado wako hai.

Polisi wapata ajali wakimkimbiza muuza Gongo, wanne wafariki
Ampiga mapanga Muhubiri aliyempa unabii wa uongo