Watu wanne wamepoteza maisha eneo la Chwele, Bungoma nchini Kenya, kufuatia kutokea kwa ajali iliyohusisha gari la Polisi lililokuwa likikimbiza mchuuzi wa Pombe haramu ya Gongo, kugongana na Pikipiki.

Kwa mujibu wa Watu walioshuhudia mkasa huo, wamesema gari hilo la Polisi lilikuwa likimkimbiza mwendesha pikipiki aliyekuwa akisafirisha chang’aa (Pombe haramu ya Gongo), kuelekea eneo la Kimilili na kupelekea watu watatu kufariki papo hapo.

‘Tumekerwa sana na kitendo hiki ambapo polisi wamesababisha vifo vya watu wetu, naomba mamlaka zinazohusika zichukue hatua, zifanye uchunguzi na kuadhibu kisheria polisi waliohusika,” alisema mmoja wa mashuhuda, Abiud Wekesa.

Amesema. mtu wa nne alifariki wakati akiendelea kupokea matibabu katika Hospitali ya Chwele na kufanya idadi ya jumla ya waliofariki kutokana na utepetevu wa askari kuwa wanne.

Wizara ishirikishe wadau utafiti Sayansi ya Bahari - Dkt. Mpango
Aliyedaka penati ya Pele afunguka, aonesha mpira wa tukio