Uingereza, Norway na Marekani zimetaka pande zote zinazopigana nchini Sudan Kusini kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, limesema kuwa mabalozi wa nchi hizo walitoa wito huo katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba.
Aidha, makubaliano ya mwezi uliopita yalikuwa na lengo la kusitisha mapigano yaliyodumu kwa muda wa miaka minne, ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu wasiokuwa na hatia.
Hata hivyo, Marekani, Uingereza na Norway, ziliunga mkono makubaliano ya mwaka wa 2005 yaliyopelekea uhuru wa Sudan Kusini kutoka kwa Sudan na zimetishia kuweka vikwazo vya pamoja au vya nchi binafsi dhidi ya pande itakayokiuka makubaliano ya kusitisha mapigano.