Katibu wa baraza la mawaziri nchini Japan ,Yoshihide Suga anatarajia kuzunguza na vyombo vya habari kuhusu uchaguzi wa mrithi wa waziri mkuu Shinzo Abe ambaye pia ndiye kiongozi wa chama cha Liberal Democratic Party (LDP).
Suga anahitisha mkutano na vyombo vya habari kwa lengo la kuthibitisha mpango wake kuwania nafasi hiyo.
Msaidizi huyo wa muda mrefu wa waziri mkuu Abe, amekuwa akitajwa kuwa kwenye nafasi nzuri ya kushika nafasi ya kuongoza chama cha LDP na waziri mkuu wa taifa hilo .
Wiki moja iliyopita Abe alitangaza maamuzi yake ya kujiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya.
Suga anakabiriwa na upinzani mkali toka kwa aliekuwa waziri wa ulinzi, Shigeru Ishiba, na waziri mstaafu wa mambo ya kigeni Fumio Kishida,