Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya nchini kuwa karibu na kutoa misaada kwa Wananchi wanaokumbwa na mafuriko na wakati wa majanga.

Waziri Mchengerwa ametoa agizo hilo mara baada ya kutebelea ma kujionea hali ilivyo katika eneo la jangwani linalokubwa na mafuriko mara kwa mara.

Hata hivyo, Mchengerwa amethibitisha kwamba ujenzi wa daraja kubwa utaanza mapema mwakani kwa lengo la kukabiliana na changamoto za mafuriko.

Naye Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, amewataka watendaji wa wakala wa Barabara Tanroad na Wakala wa Barabara Vijijini – TARURA, kufanya mapitio ya barabara wakati wa msimu wa mvua na kuagiza kuondolewa kwa tope chini ya daraja la Jangwani.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameendeleza zoezi la kuondoa mchanga kama hatua za dharura. Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROAD, Mhandisi Dorothy Mtenga, na Mratibu wa Mradi kutoka Benki ya Dunia, Injinia Humphrey Kanyenye, wamethibitisha kuwa ujenzi utazingatia pia utunzaji wa mazingira.

RC Mrindoko akemea Viongozi kuchochea mgogoro wa Ardhi
Mapambano Dawa za kulevya: Tunahitaji ushirikiano - Dkt. Rioba