Sungura mwenye urefu wa futi nne aliyeshinda tuzo anadhaniwa kuwa ameibiwa kutoka katika boma lake.
Sungura huyo kwa jina Darius, ambaye ni ”mkubwa zaidi duniani” alitoweka kutoka katika nyumba yake iliyopo eneo la Stoulton, Worcestershire, Uingereza Jumamosi usiku.
Mmiliki wake Annette Edwards ametoa pauni 1,000 sawa na fedha za kitanzania shilingi Milioni Tatu, Laki moja Themanini na tano elfu na mia tisa tisini na mbili (3185992.93), kama zawadi kwa atakayemrudisha kwake na akasema ni “siku ya huzuni sana “.
Akiwa na urefu wa sentimeta 129 (au futi 4 ), Sungura Darius ndiye anayeshikilia rekodi baada ya kutajwa kama sungura mrefu zaidi duniani kwa mwaka 2010.
Polisi katika kituo cha West Mercia alisema kuwa inaaminiwa kuwa Darius aliibiwa kutoka kwenye ua lake, ambao upo katika bustani ya mmiliki wake, usiku Jumamosi.
Bi Edwards alisema kuwa Darius ni “mzee sana hawezi kuzaa sasa ” na akaomba sana aliyemchukua amrejeshe salama.
Alitajwa kama sungura mrefu kuliko wote duniani na Guinness World Records mwezi Aprili mwaka 2010, wakati alipopimwa kwa ajili ya gazeti la Daily Mail.
Bi Edwards alisema kuwa alipata tuzo hiyo kutoka kwa Alice, na ilikuwa ni tuzo ya nne ya sungura huyo.
Hili si jambo geni sana kwa Watanzania kwani mapema Mwezi Machi mwaka huu Msanii maarufu wa filamu nchini, Wema Sepetu alimpoteza mbwa wake aliyefahamika kwa jina la Manunu ambapo Wema alitoa ahadi ya Shilingi Milioni mbili kwa ambaye angemrejesha mbwa huyo.