Rais Dkt. John Magufuli ameelezea jinsi Rais wa awamu ya tatu Hayati Benjamin Mkapa alivyoanzisha na kuweka mkazo mkubwa wa kuimarisha taasisi na mifuko ya jamii ili kukuza uchumi wa nchi na kuwaondoa watanzania katika umaskini ambapo ametaja sekta ya afya, sekta ya maji pamoja na sekta ya elimu.
Katika sekta elimu alianzisha Mpango wa Maendeleo ya Msingi (MEM), Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MES),Baraza la elimu ya mitihani (NECTA), bodi ya mikopo (HESLB), kamisheni ya Vyuo vikuu (TCU), Baraza la taifa la elimu ya ufundi (VETA), Mamlaka ya elimu Tanzania (TEA).
Katika kukabiliana na umasikini alianzisha Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge (MKURABITA), Mpango wa Mkakati wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini Tanzania (MKUKUTA) na Mpango wa kusaidia kaya masikini Tanzania (TASAF).
Pia alianzisha Baraza la biashara Tanzania (TNBC) Sekta binsfi NBC pamoja na NMB, bodi ya mfuko wa barabara (ROAD FUND na TANROAD),Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA), Taasisi ya kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mpango wakupambana na ugonjwa wa ukimwi (TACAIDS).
Halikadharika alianzisha Chama cha hati miliki (COSOTA), wakala wa majengo (TBA) Wakala wa usaji (RITA) Wakala wa uslama (OSHA) wakalawa serikali wa ndege (TGFA), wakala wa usajili wa leseni za biashara (BRELA), Mamlaka ya hali ya hewa (TMA), Mamlaka ya usalaama wa anga (TCAA)
Ambapo Rais Magufuli amesema kuwa haya yote yalifanyika kutokana na kuundwa na kutunga sheria namba 30 ya mwaka 1997 iliyosaidia kuanzisha wakala mbalimbali ambao wananendelea kufanaya kazi mbalimbali katika nchi yetu.
Amesema kuwa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa alianzisha Taaasisi ya mkapa Faundation ambapo mara baada ya kustaafu taasisi hiyo imeeendelea kushirikiana vyema na serikali .
”Mkapa faundation imeajiri watumishi wa afya 3004 imekarabati maabara ya vituo vya afya13 imejenga majengo ya upasuaji 11, na pia nyumba za watumishi wa afya zipatazo 482” amesisitiza Rais Maagufuli.