Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussien Ali Mwinyi amesema Taasisi za dini nchini zina mchango mkubwa kwa Serikalini ili kufanikisha kuendeleza amani.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu mjini Zanzibar, wakati alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Jumuiya Sunni Jamaat, walipofika ofisini kwake hii leo Februari 2, 2023 kujitambulisha.

Amesema, taasisi hizo zinawalea vijana kiimani, kiweledi, kiujasiri na kiuzalendo kwa manufaa ya Taifa na viongozi wao, jambo ambalo linaimarisha amani na uthubutu wa kuyafikia maendeleo.