Rais wa Kampuni ya Utengenezaji wa Mabehewa ya Sung Shin Rolling Stock Technology (SSRT) ya Nchini Korea, Gye Shul Park, ameonesha nia ya kujenga Kiwanda cha kuunga Mabehewa hapa nchini, ambayo itaweza kuleta ajira kwa Watanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kampuni ya Utengenezaji wa Mabehewa ya Sung Shin Rolling Stock Technology (SSRT) ya Nchini Korea Gye Shul Park na Ujumbe wake uliofika Ikulu Chamwino- Dodoma.

Gye Shul Park, ameonesha nia hiyo hii leo Februari 2, 2023 mara baada ya kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na na Ujumbe wake uliofika Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Kampuni ya Utengenezaji wa Mabehewa ya Sung Shin Rolling Stock Technology (SSRT) ya Nchini Korea, Gye Shul Park aliyeambatana na Ujumbe wake uliofika Ikulu Chamwino – Dodoma hii leo Febuari 2, 2023.

Ujenzi wa Kiwanda hicho cha mabehewa, si tu utaweza kutoa ajira kwa Watanzania lakini pia utasaidia kuongeza Pato la Taifa, kuimarisha sekta ya usafiri na usafirishaji na kuzinufaisha nchi jirani kiuchumi.

Majaliwa asisitiza weledi, miiko utumishi wa Umma
Robertinho: Tutashambulia tu