Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliviera amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa 22 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Stars.

Simba SC itakua nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa, ikiweka malengo makubwa ya kusaka ushindi kwenye mchezo huo, ili kuendelea kuifukuzia Young Africans kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu.

Kocha Robertinho ametoa uhakika wa utayari wa kikosi chake alipozungumza na Waandishi wa Habari leo Alhamis (Februari 02) jijini Dar es salaam.

“Tunategemea kupanga kikosi kamili kwakuwa tunaenda kukutana na timu Bora. Tutacheza kwa kufuata falsafa za Simba, tunashambulia na kukaba kwa pamoja lakini lengo letu ni kuhakikisha tunapata pointi tatu”

“Nimewaandaa vizuri wiki hii katika soka kila kitu kinawezekana. Simba SC wana falsafa nzuri ya kushambulia na ni eneo zuri wachezaji kuonyesha ujuzi mimi pia napenda soka la kushambulia na kushinda.”

“Mipango ni kwamba cheza kwa nguvu ukiwa na mpira au bila mpira na kushinda”

“Nina Benchi zuri la ufundi wamenijuza kuhusu Singida. Ninawaheshimu na mechi ni mechi lakini kesho matumaini yangu ni kucheza vizuri na kushinda” amesema Robertinho

Mwanga fursa za ajira, uimarishaji wa uchumi wachomoza
Bares: Tutashirikiana kuinusuru Prisons