Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeweka wazi kuwa mpango wapeleka mahakamani kesi 36 za rushwa zinahusisha masakata mbalimbali nchini, maarufu kama majipu.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna Valentino Mlowola ameeleza hayo jana alipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Moja kati ya kesi wanazotarajia kuzifikisha mahakamani, inahusu kampuni ya Mafuta ya Lake Oil ambayo inadaiwa kufanya udanganyifu kwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa umma wasio waaminifu kuwasaidia kukwepa kodi ya zaidi ya shilingi Bilioni 8.5.

Kamishna Mlowola alisema kuwa Lake Oil ilifanya udanganyifu na kuuza nchini lita 17,461,111 za mafuta ya Petrol yaliyokuwa yanapaswa kusafirishwa kwenda Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo kupitia Zambia. Hivyo, ilikwepa kulipa kodi ya kiasi hicho kikubwa cha fedha.

Aliwatahadharisha watumishi wote wa umma nchini kuhakikisha hawajihusishi na vitendo vya rushwa kwani hawatasalimika. Alisema kuwa Taasisi hiyo itamshughulikia mtu yeyote bila kujali cheo chake kwa kuwa anaripoti moja kwa moja kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

“Bahati nzuri mimi nina ripoti moja kwa moja kwa ‘Mtumbua Majipu’ mwenyewe,” alisema.

Picha ya kiazi yauzwa kwa zaidi ya shilingi bilioni mbili
Uhaba: Serikali yaagiza wanaume kuoa wanawake zaidi ya wawili au kufungwa jela maisha