Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), imeokoa zaidi ya shilingi bilioni moja na kuzirejesha serikalini na kwenye vyama vya ushirika.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu taarifa ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2020/2021 ya taasisi hiyo.