Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mwanza, inawashikilia wafanyakazi 30 wa bohari ya dawa (MSD), na mfanyakazi mmoja wa wizara ya afya kwa tuhuma na ubadhilifu wa dawa na vifaa tiba.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza, Emmanuel Stenga, amesema wafanyakazi wanashikiliwa kwa tuhuma hizo ambazo zimepelekea ubadhilifu wa zaidi ya shilingi milioni 254.
Amesema watuhumiwa hao bado wapo chini ya ulinzi na wanaendelea kuhojiwa, kwa watakao thibitika watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Aidha ametoa wito kwa wafanyakazi kuridhika na vipato vyao na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa ofisini au kupiga simu ya dharula namba 113.