Kutokana na utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya UKIMWI, umeonesha kuwa mlipuko wa virusi vya corona una athari katika upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya VVU (ARV’s).

Imeelezwa kuwa hiyo ni kutokana na watu kubaki ndani na mipaka kufungwa ambako kumeleta changamoto katika uzalishaji na usambazaji. Na itasababisha uhaba wa upatikanaji ikiwemo kuisha kwa akiba katika miezi 2 ijayo na gharama kupanda.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Winnie Byanyima ametoa wito kwa nchi zote na wanunuzi wa dawa hizo kuchukua hatua ili kuokoa maisha na kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya VVU.

Jumla ya watu milioni 24.5 wanatumia dawa za VVU tangu mwishoni mwa mwezi Juni mwaka 2019. Aidha, tafiti imeonesha nchi za kipato cha kati na chini ndizo zitakazoathirika zaidi.

Mahujaji wachache kuingia Saudi Arabia mwaka huu
Raia wa Malawi wapiga kura za marudio kumchagua Rais