Juhudi kubwa zimekuwa zikifanywa na wahandisi na mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), kurejesha miundombinu iliyoathiriwa na mvua zilizonyesha kwa
siku mbili mfululizo jijini Dar es Salaam na hivyo kusababisha maeneo kadhaa ya jiji kukosa umeme.
Kwa mujibu wa Mhandisi Mkuu wa TANESCO Kinondoni Kaskazini Mhandisi, Godlove Mathayo, amesema kuwa mafundi wanafanya jitihada kusimika nguzo kwaajiri ya kukabiliana na uharibifu wa miundo mbinu uliojitokeza hasa katika huduma ya Nishati ya umeme.
“Baada ya matengenezo hayo yanayoendelea sasa, wakazi ambao wanategemea kupata umeme ni wote wa maeneo ya Kwa Malecela, Victoria na Kawe kwa maana ya eneo la Mbezi Chini.” amesema Mathayo.
Kwa upande wake Kaimu Meneja Uhusioano, Leila Muhaji, amewaomba radhi wateja walioathirika kutokana na hitilafu hiyo na kuwasihi kuwa wavumilivu kwani mafundi wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha umeme unarejea katika hali yake ya kawaida.
-
Mwanri azicharukia halmashauri Tabora
-
Serikali yawatahadhalisha Wafugaji
-
Naibu Waziri wa Nishati atembelea kituo cha kusambaza Umeme
Hata hivyo, Miundombinu ya jiji Dar es salaam imeathirika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivyo amewataka wananchi wasisogelee miundombinu ya umeme wanapoona nguzo imelala au waya umelala wasiguse na watoe taarifa kwa mafundi umeme.