Tanzania na China zimekubaliana kuendeleza mahusiano ya kimkakati baina yao ili kuwezesha uwepo wa ulingo sawa miongoni mwa mataifa katika kusimamia maslahi na maendeleo ya nchi husika katika jumuiya za kimataifa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John kabudi leo jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke

Ambapo amesisitiza umuhimu wa mataifa kuheshimiana na kutokubali kuingilia uhuru wa mambo ya ndani ya nchi kwa kisingizio cha haki za binadamu, demokrasia ama jambo lolote lingine.

Ameongeza kuwa mazungumzo hayo ya kimkakati yamelenga kutambua kuwa mwaka huu ni mwaka wa 55 tangu Tanzania na China zisaini mkataba wa urafiki ambao uliweka msingi wa mahusiano makubwa na ya dhati katika nyanja za ulinzi, usalama, afya, kilimo, elimu na miundo mbinu.

Kwa upande wake Balozi wa China hapa Nchini Wang Ke amesema China wakati wote ni Rafiki mwaminifu na wa kudumu wa nyakati zote kwa Tanzania na kwamba kutimiza miaka 55 ya urafiki wa nchi hizo ni kielelezo tosha na siku zote wataendelea kuuheshimu na kuuenzi urafiki huo.

WFP waibuka kidedea tuzo ya amani nobel 2020
Sababu ya Rais Chakwera kukatisha ziara yake Tanzania