Shirika lisilo la kiserikali la Health Promotion Tanzania (HDT), limetoa wito kwa benki zilizoikopesha Tanzania kuisamehe au kuiondolea riba katika madeni yake ili fedha zilizotakiwa kulipa deni hilo zielekezwe kwenye sekta ya afya kwa kuimarisha mifumo ya afya nchini.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Dkt. Peter Bujari wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 1, 2020 kuhusu kampeni wanayofanya ya kupaza sauti Tanzania kusamehewa madeni inayotakiwa kulipa.
Bujari amesema kuwa ni muhimu benki hizo kutafakari kuhusu suala hilo katika vikao wanavyotarajia kukaa siku zijazo, baadhi ya mabenki yanayoikopesha Tanzania ni pamoja na IMF, World Bank, Benki ya Afrika, pamoja na benki ya Exim ya Korea.
Aidha ametoa wito kwa serikali kuwa endapo itasemehewa ni vyema wakawekeza kwenye sekta ya afya kwa kuimarisha mifumo ya afya na kujiweka tayari kupambana na milipuko ya magojnwa inayoweza kujitokeza.