serikali za Tanzania, Malawi zipo kwenye mazungumzo ya kushirikiana katika ukuzaji wa sekta ya usafirishaji wa nchi zote mbili.
Akizungumza baada ya kuwasili ikulu jijini Dar es Salaam Rais wa Malawi Dokta Lazarus Chakwera amesema kuwa yeye na mwenyeji wake Dokta John Magufuli wapo kwenye mazungumzo ya mikataba juu ya kukuza na kurahisisha usafirishaji wa watu na mizigo baina ya nchi hizo .
” Tunaangalia makubaliano na mikataba mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha shughuli ya Tume ya pamoja ya ushirikiano ili tuweze kurahisisha zaidi usafiri wa Watu na mizigo pamoja na huduma kwa haraka zaidi” amesema Chakwera.
Aidha rais Chakwera amesema kuwa mwenyeji wake amempatoa wito kwa watu wa malawi kutumia bahari na bandari ya Mtwara kufika Dar es Salaam.
“Kaka yangu Magufuli ameniambia tusijifikirie kama tuko mbali na Bahari, tunaweza kuifikia Bahari kupitia Bandari ya DSM na Mtwara”.
kwa upande wake rais Magufuli amesema kuwa amefurahi kuzungumza na Chakwera kwakuwa anayoyazungumza yanaakisi upendo wa taifa la malawi kwa Tanzania .
“Tumezungumza kwa raha sana na Mh Rais, na nimemuona sura na moyo wake vina-reflect upendo kwa wana Malawi na Tanzania, na niliona kweli huyu baba ana maono ya kiaskofu na mimi nimejifunza kwake mambo mengi” amesema Magufuli
Rais Chakwera yupo katika ziara ya siku tatu hapa nchi.