Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limetoa orodha mpya ya viwango vya soka duniani baada ya kuchezwa kwa mechi za kufuzu kwa kombe la Dunia 2018 huku Kenya na Tanzania zikishuka zaidi ya hatua 10 kwenye orodha hiyo.
Katika orodha mpya ya FIFA Tanzania inashika nafasi ya 136 kwa sasa baada ya kushuka nafasi 11, Kenya nayo imeshuka nafasi 14 hadi nafasi 102.
Nchi nyingine katika ukanda wa Afrika Mashariki ni Uganda iliyopanda hatua moja hadi nafasi ya 70 Burundi ikisalia katika nafasi ya 129.
Malawi imeshuka nafasi moja hadi nambari 117 ambapo inafuatiwa na Rwanda iliyo katika nafasi ya 118, DR Congo wamepanda nafasi 7 hadi nafasi ya 35.
-
Icardi aiongoza Inter Millan kuilaza Ac Millan
-
Jose Mourinho asema hatastaafu akiwa Man Utd
-
Federer ang’ara michuano ya Shangai Masters
Ujerumani bado wanaongoza wakishika nafasi ya kwanza kwa ubora duniani wakifuatwa na Brazil wanaoshika nafasi ya pili. Ureno ni ya tatu na nafasi ya nne ni Argentina.
Afrika Tunisia wanaongoza wakiwa nafasi ya 28 duniani baada ya kupanda hatua 3 wakifuatwa na Misri walio nafasi ya 30 duniani.