Tanzania imeendelea kuporomoka katika viwango vya ubora wa soka duniani baada ya shirikisho la soka la kimataifa FIFA kutoa orodha ya viwango vya mwezi Novemba hii leo.
Orodha ya viwango hivyo inaonyesha Tanzania inashika nafasi ya 142, wakati Uganda ikieendelea kuongoza kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, ikiwa inashika nafasi ya 15, wakati Senegal sasa inaongoza kwa Afrika nzima.
Hata hivyo Tanzania imeporomoka kwa nafasi sita ikitokea nafasi ya 136 mwezi uliopita, huku ikikumbukwa mwanzoni mwa mwezi huu, Taifa Stars ililazimisha matokeo ya sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Benin ugenini, na iliaminika huenda ingesalia katika nafasi yake ama kupanda kwa nafasi kadhaa.
Wakati Tanzania ikishuka katika viwango vya ubora wa soka duniani, 10 Bora viwango hivyo kwa mwezi huu inaonyesha kuwa Ujerumani inaongoza ikifuatiwa na Brazil, Ureno, Argentina, Ubelgiji, Hispania, Poland, Uswisi, Ufaransa na Chile.