Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt. Switbert Mkama amesema katika kukabiliana na changamoto ya ukame, Tanzania imefaidika na miradi ya kuhamasisha matumizi endelevu ya ardhi hivyo kupunguza kuenea kwa hali ya jangwa na ukame na athari zake.

Mkama ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha wataalamu cha kuhakiki rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Kupambana na Kuenea kwa hali ya Jangwa na Ukame chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa hali ya Jangwa na Ukame (UNCCD) leo Januari 25, 2023 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Catherine Bamwenzaki akifungua kikao cha wataalamu cha kuhakiki rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Kupambana na Kuenea kwa hali ya Jangwa na Ukame chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa hali ya Jangwa na Ukame (UNCCD), Januari 25, 2023 jijini Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya Naibu Mkuu, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Catherine Bamwenzaki amesema Mkoa wa Kilimanjaro unafaidika na mradi wa kuongoa maeneo yaliyoharibibika wakati Tabora na Katavi imefaidika na mradi wa kuhifadhi misitu ya miombo.

Amebainisha kuwa Tanzania inafaidika pia na Mradi wa Kunusuru Vyanzo vya Maji Kupitia Usimamizi Endelevu wa Ardhi Katika Mabonde Madogo ya Ruvu na Zigi, Mradi wa Kurejesha Ardhi Iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula Katika Maeneo Kame ya Tanzania pamoja na Programu ya kuandaa Shabaha ya kuzuia uharibifu wa ardhi ifikapo mwaka 2030.

Kenyatta ataka suluhisho mgogoro wa DRC, Rwanda
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 26, 2023