Kufuatia kusambaa kwa kipande cha video kikimuonesha Mwalimu akiwachapa wanafunzi fimbo za miguuni wakiwa wamevua viatu, Serikali imelizungumzia tukio hilo ikiwemo kuchukua hatua za kumsimamisha kazi Mwalimu huyo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akizungumzia tukio hilo amesema, uchunguzi juu ya tukio hilo unaendela na hatua stahiki zitachukuliwa ili kubaini na kukomesha vitendo vya namna hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Makundi Maalumu, Dk Doroth Gwajima amewataka wananchi kutoa taarifa wanapoona matukio ya namna hiyo, ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa wahusika.

Tukio hilo, linadaiwa kutokea Januari 10, 2023 katika Shule ya moja ya Msingi iliopo Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera, na kipande cha video kinamwonesha mwalimu akiwakanyaga miguuni huku akiwachapa Wanafunzi ambao walisikika wakilia na kuomba msamaha.

Phiri, Inonga mambo safi Simba SC
Teuzi na panga pangua ya Wakuu wa Wilaya, Shaka aibukia Kilosa