Wachezaji Moses Phiri na Henock Inonga Baka wamerejea katika maozezi ya pamoja na Wachezaji wenzao wa Simba SC, baada ya kuwa nje ya Uwanja tangu Desemba-2022 kutokana na kuwa majeruhi.

Phiri ambaye ni Kinara wa upachikaji magoli kwenye Klabu hiyo, aliumia mguu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Desemba 21, Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na timu hizo kupata sare ya 1-1.

Inonga alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons uliofanyika Desemba 30, Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam, huku Simba SC ikiambulia ushindi wa 7-1.

Wawili hao wameonekana wakiwa kwenye mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumamosi (Januari 28).

Kwa upande wa Kiungo Mshambuliaji Peter Banda ambaye nae alikaa nje ya Uwanja tangu Novemba 9-2022, kufuatia kuumia kifundo cha mguu katika mchezo dhidi ya Singida Big Stars, ameendelea na mazoezi baada ya kuonekana Dubai akifanya mazoezi ya pekee yake wakati timu hiyo ilipoweka kambi ya siku Kumi huko Falme za Kiarabu.

Polisi yajipanga kiusalama ujio wa Lissu
Aliyewapiga Wanafunzi asimamishwa kazi