Tanzania na Zimbabwe zimetiliana saini hati tano za makubaliano ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwa ni kutekeleza maelekezo ya Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ya kuhakikisha nchi hizo zinashirikiana katika masuala ya kiuchumi.

Hati hizo za makubaliano zimesainiwa Harare nchini Zimbabwe na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi, kwa upande wa Tanzania na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Zimbabwe Luten Jenerali Mstaafu Sibusiso Moyo.

Akizungumza mara baada ya kusaini hati hizo za makubaliano Waziri Kabudi amesema kuwa mkutano huo unafanyika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 21, na kuongeza kuwa uhusiano baina ya Tanzania na Zimbabwe ulianza kabla ya ukoloni.

Hata hivyo, Makubaliano hayo yameafikiwa katika nyanja za ushirikiano wa biashara, uchumi na uwekezaji, siasa na diplomasia, utalii, uwezeshaji wa wanawake na masuala ya jinsia pamoja na masuala mbalimbali.

Mtoto wa Osama, Hamza Bin Laden Ameuawa
Video: Mo Dewji chapa kazi usiwe mnyonge, songa mbele -JPM